Habari za Mastaa

Roma kafunguka kuchelewa kurudi bongo “Waniweke kwenye sala zao”

on

Mkali wa Hip Hop bongo Roma Mkatoliki anayetamba na wimbo ‘Anaitwa Roma’ , amefunguka sababu za yeye kushindwa kurejea Tanzania kwa wiki nne tangu aende Marekani huku akikanusha taarifa za kuwa wimbo wake mpya ndio sababu ya yeye kuogopa kurejea nchini.

Ni zaidi ya wiki tatu sasa toka msanii huyo aende nchini Marekani na kuonekana katika shughuli mbalimbali nchini humo hali ambayo iliibua maswali ya kwanini hajarejea nchii Tanzania..?

Sasa kupitia kipindi cha Top 20 ya Clouds Fm siku ya Jumapili ya Desemba 15, 2019 Roma ameeleza kuwa sababu kubwa iliyompeleka marekani ni mualiko maalum alioupata kutoka kwa jamii ya watu wanaozungumza Kiswahili wanaoishi marekani maarufu kama SUSA (Swahili society USA) mualiko ambao ameeleza kuwa aliupata kama msanii wa Tanzania anayetumia Kiswahili katika kazi zake za kufikisha ujumbe kwa Jamii husika ambapo tamasha hilo hufanyika kila mwaka.

BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA VIDEO.

DU!! HAMISI ALIVYOKISS NA MSHIRIKI MWENZAKE MBELE YA MAJAJI WA BSS

VIDEO: Mama yake Ben Pol akicheza zilipendwa baada ya mwanae kuwa DJ wa muda

Soma na hizi

Tupia Comments