AyoTV

VIDEO: Mastaa wa Bongo walivyoguswa na mkasa wa Roma na wenzake

on

Tukio la kutekwa kwa Rapa Roma Mkatoliki na wenzie watatu liliripotiwa usiku wa April 5, 2017 ambapo watu wasofahamika walivamia studio za Tongwe Records na kuondoka nao kuelekea kusikojulikana.

Kufuatia tukio hilo wasanii mbalimbali Tanzania walikutana Coco Beach Dar es Salaam kujadili namna ya kumtafuta Roma na wenzake huku Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikitoa taarifa ya kushtushwa na kuahidi kushirikiana na wasanii na Jeshi la Polisi kuwatafuta.

Sasa basi, kutokana na kuguswa kwao na tukio hilo na kukosekana taarifa zozote hadi sasa kuwahusu watu hao, wasanii mbalimbali wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kueleza hisia zao.

Bonyeza play kutazama…

VIDEO: Wasanii walivyokutana Coco Beach kwa ajili ya kumtafuta Roma. Bonyeza play kutazama. 

Soma na hizi

Tupia Comments