Karibu kwenye kalamu au KKK ni jina la single mpya ya Roma Mkatoliki ambayo ina siku kadhaa ambapo Roma amezungumza na millardayo.com na kueleza baadhi ya matukio aliyokutana nayo kutokana na hii single.
Kama umeisikiliza KKK, ni single ambayo kidogo ina maneno makali ambapo kuna taarifa ilitoka kuwa mara baada ya mama yake mzazi kuusikia wimbo huu alimnunia Roma kwa siku 4.
Roma ameanza kwa kusema >>> ‘Kweli mama alivosikia KKK alichukia sana na kuniuliza kwanini nimetukana kwenye wimbo basi baada ya hapo kila nikimpigia akawa hapokei simu zangu karibu siku 4’.
Kwenye mstari mwingine Roma anasema KKK ndio single yake ambayo mpaka sasa inamshangaza kutokana na aina ya matukio yanayojitokeza ikiwemo ile ya madereva boda boda na Bajaj kumfata mpaka kwenye studio ilikotengezwa hiyo single kuomba wawekewe kwenye flash na memory card zao kwa ajili ya kusikiliza.