Michezo

Cristiano Ronaldo ataondoka Real Madrid? Zidane karudia maneno haya …

on

Cristiano Ronaldo amerudi tena kwenye headlines baada ya weekend kufunga goli nne peke yake katika ushindi wa goli 7-1 dhidi ya klabu ya Celta Vigo, goli hizo hizo alizofunga Ronaldo hakuzichukulia poa kocha wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane.

Zidane ambaye amejiunga na timu A ya Real Madrid kuchukua nafasi ya Raphael Benitez, amezungumza na kusisitiza kwa mara nyingine tena kuwa Real Madrid wanahitaji kuendelea kumbakiza kikosini Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akihusishwa kutaka kuhama.

450223068_3154629

Baada ya Ronaldo kufunga goli nne peke yake dhidi ya Celta Vigo, anakuwa mchezaji wa kwanza Ulaya kufunga jumla ya goli 350 akiwa na klabu moja kwa muda mfupi. Hii sio mara ya kwanza Zidane anazungumza kuhusu kauli za kumuhitaji Ronaldo, kitu ambacho kinahisiwa kuwa huenda akawa ana mipango ya kuondoka.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER  FB  YOUTUBE

Tupia Comments