Michezo

Zifahamu rekodi tatu za Ronaldo baada ya hat-trick yake ya April 12 2016

on

Jina la staa wa soka wa kimaifa wa Ureno Cristiano Ronaldo lilirudi kwenye headlines baada ya usiku wa April 12 2016 kuisaidia klabu yake ya Real Madrid kufuzu hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuifungia hat-trick dhidi ya Wolfsburg.

Baada ya hat-trick hiyo Ronaldo ameweka rekodi kadhaa ndani ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na nje ya Ligi hiyo, Ronaldo ndiye mchezaji anashikilia rekodi ya kufunga magoli zaidi ya 30 katika misimu sita ya Laliga mfululizo, hat-trick ya jana imemfanya Ronaldo kuweka rekodi ya kufunga zaidi ya goli 45 katika kila msimu akiwa na Real Madrid.

Kama ulikuwa hujui Ronaldo anashikilia rekodi ya kufunga jumla ya goli 17 katika msimu 2013/2014 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya idadi ambayo haijafikiwa na mchezaji yoyote, ila headlines mpya ni kuwa Ronaldo anakaribia kuvunja rekodi hiyo msimu huu, kwani hadi sasa amefunga jumla ya goli 16.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments