Michezo

Ronaldinho aliwekewa kipengele cha kwenda Night Club mara 2 kwa wiki

on

Mshambuliaji wa zamani wa club ya FC Barcelona na Flamengo Ronaldinho Gaucho imegundulika kuwa wakati akichezea club ya Flamengo ya kwao Brazil alikuwa na kipengele maalum katika mkataba wake.

Ronaldinho ambaye alikuwa ni staa mwenye kupenda starehe alikuwa na kipengele katika mkataba wake na Flamengo kinachomruhusu kwenda Night Club mara mbili kwa wiki, hii ni tofauti na sheria za club nyingi za soka.

Staa huyo alijiunga na Flamengo 2011 baada ya kuwa na misimu mitatu katika club ya AC Milan, mkataba wa Ronaldinho ulieleza kuwa utavunjika endapo Flamengo hawatokubali matakwa yake ya ziada ikiwemo kwenda Night Club.

Ronaldinho alicheza mwaka mmoja katika club ya Flamengo na kufanikiwa kufunga magoli 19 na kutoa assist 13.

Soma na hizi

Tupia Comments