Michezo

Rekodi nyingine kwa Cristiano Ronaldo hii hapa mtu wangu…

on

ronaldo3Usiku wa jana jumatano Cristiano Ronaldo ambaye kwa sasa ndiye mchezaji bora wa dunia ameandika historia nyingine ndani ya klabu yake ya Real Madrid.

Akiwa tayari amecheza mechi 288 tangu ajiunge na klabu hiyo, Ronaldo ambaye ni raia wa Ureno aliweza kuisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 huku akifunga bao moja ambalo limehitimisha idadi ya mabao 300 ambayo tayari amefunga tangu ajiunge na Real.

ronaldo

Ronaldo alifunga bao lake la 300 wakati Real Madrid ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Rayo Valcono iliyokuwa nyumbani katika uwanja wake wa Teresa Rivero katika mechi ya La Liga.

ronaldo2

Bao la pili la Real lilifungwa na James Rodriguez.

puto

Naye Mbrazil, Philippe Coutinho ameisaidia klabu yake ya Liverpool kupata ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Blackburn Rovers na sasa imesonga hadi nusu fainali ya Kombe la FA.

Ushindi huo umeamsha matumaini ya Liverpool kubeba kombe angalau kombe moja msimu huu, na sasa itakutana na Aston Villa Aprili 19.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments