Club ya Man United imetangaza kuwa staa wao wa Ureno Cristiano Ronaldo hatorejea mazoezini leo kuanza maandalizi ya msimu mpya wa 2022/2023 kwa sababu za kifamilia.
Leo wachezaji wote waliokuwa mapumzikoni baada ya michezo ya kimataifa walipaswa kurejea kuanza mazoezi ila Ronaldo zinadaiwa kuwa ana mpango wa kuondoka Man United.
Kocha wa Man United Erik Ten Hag ameripotiwa kuwa anahitaji huduma ya Ronaldo ambaye ana mkataba hadi mwisho wa msimu wa 2022/23 na una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Taarifa za ndani zinaeleza Ronaldo ambaye ni mshindi mara tano wa UEFA Champions League, anataka kuondoka sababu ya Man United kushindwa kufuzu kucheza UEFA Champions League msimu ujao, michuano ambayo amekuwa akicheza kwa miaka 19 mfululizo sasa.