Mshambuliaji wa Cameroon Vincent Aboubakar amefunguka kuhusu kuondoka kwake Al Nassr baada ya Cristiano Ronaldo kujiunga na klabu hiyo.
Cristiano Ronaldo alijiunga na Al Nassr kwa mkataba wa bure Desemba 2022 baada ya kukamilisha kuondoka kwake Manchester United.
Ujio wa Ronaldo ulimaanisha kwamba Al Nassr alilazimika kumwachia mchezaji mmoja wa kigeni ili kutoa nafasi ya usajili wake na Vincent Aboubakar ndiye mchezaji aliyetoa nafasi kwa icon huyo wa Ureno.
Licha ya ripoti kuwa Ronaldo alimlazimisha kuondoka Aboubakar, ambaye sasa anachezea Besiktas ya Uturuki, anasisitiza kuwa hilo ni mbali na ukweli.
“Kwa ujio wa Cristiano, nilimweleza kocha kabla ya kuwasili kwake kwamba tayari nilitaka kuondoka. Ronaldo alipofika, ilibidi mchezaji wa kigeni aachiliwe,” Aboubakar alisema kwenye kituo cha televisheni cha Ufaransa Canal+. (kupitia DailyMail)
“Ronaldo aliniomba kubaki na klabu ilitaka nibaki angalau hadi mwisho wa msimu, lakini nilitaka kuondoka. Klabu ilinitaka nibaki na ilikuwa tayari kulipa mshahara wangu hadi mwisho wa msimu.”