Michezo

Pichaz za Ronaldo akiwa katika ndege binafsi akielekea kujiunga na timu yake ya taifa…

on

Ikiwa ni mapumziko mafupi ya Ligi Kuu mbalimbali duniani ili kupisha michezo kadha ya timu za taifa iliyo katika kalenda za FIFA, Real Madrid ya Hispania ilimaliza mechi yake ya weekend kabla ya kwenda mapumziko mafupi dhidi ya Atletico Madrid na mechi kumalizika kwa sare ya goli 1-1, mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo amekodi ndege binafsi kwenda kujiunga na timu yake ya taifa.

Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa anahitaji goli moja tu ili avunje rekodi ya ufungaji wa muda wote wa klabu ya Real Madrid iliyokuwa inashikiliwa na Raul, amesafiri na ndege binafsi kuelekea kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya Ureno, ambayo itacheza mechi mbili za kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Ulaya.

2D1C4FDA00000578-0-image-a-2_1444042159245

Licha ya Cristiano Ronaldo kutofanikisha lengo lake la kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid, tayari ndio mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno ambaye ndio mfungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo, Cristiano Ronaldo ana jumla ya goli 55 alizofunga akiwa na timu yake y taifa. Lakini anatajwa kufunga zaidi ya magoli 500 ikiwa ni jumla ya goli alizofunga katika vilabu alivyochezea na timu ya taifa.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments