Michezo

Kwani Ronaldo anastaafu lini soka? nimelipata jibu leo..

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo October 14 ameingia kwenye headlines kwa mara nyingine tena ikiwa ni siku moja imepita toka aingie katika rekodi ya kushinda tuzo ya kiatu cha dhahabu mara nne.

Cristiano Ronaldo ambaye alijiunga na Real Madrid ya Hispania mwaka 2009 akitokea katika klabu ya Manchester United ya Uingereza kwa dau la pound milioni 80, kiasi ambacho kiliweka rekodi ya Dunia katika masuala ya usajili amenukuliwa na vyombo vya habari akitaja umri wake wa kustaafu soka na angependa kustaafu akiwa Real Madrid.

article-0-1E2E91FC00000578-931_634x415

Ndoto yangu ni kustaafu soka nikiwa Real Madrid kama utaweza kujitunza vizuri unaweza kucheza soka hadi ukiwa na umri wa miaka 40, nataka kuendelea kucheza kwa miaka mitano hadi sita Real Madrid, napanga kuendelea kucheza kwa kiwango changu na  wastani wangu huu wa ufungaji, najisikia vizuri Madrid na nataka kuendelea kutwaa mataji hapa>>> Ronaldo

Cristiano Ronaldo kwa sasa ana umri wa miaka 30 na mkataba na Real Madrid hadi mwaka 2018, pamoja na hayo usisahau kwamba Ronaldo siku chache zilizopita alikua akihusishwa na kutaka kurudi Man United na kujiunga na klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments