Michezo

Cristiano Ronaldo alivyojiachia kwenye mahojiano… kamtaja mpaka na atakaebeba Ballon d’Or

on

Bado headlines za staa wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid  Cristiano Ronaldo zinazidi kuchukua nafasi kila siku, hii ni sehemu ya interview ya Tv Show aliyofanya Uingereza mahali ambapo alifanya uzinduzi wa movie ya maisha yake halisi inayoitwa ‘Ronaldo’ . Katika show hiyo Ronaldo alifunguka baadhi ya vitu kuhusu maisha yake binafsi.

Katika Tv show ya ‘The Jonathan Ross Show’ Ronaldo ambaye ni mchezaji bora wa Dunia mara tatu amefunguka mambo mengi kuhusu maisha yake ila hizi ni sentensi zake tatu kuhusu ligi atazocheza baada ya Real Madrid, mahusiano yake na Lionel Messi na kuhusu mama wa mtoto wake Cristiano Ronaldo Junior.

Alipoulizwa kuhusu tuzo za mwaka huu za Ballon d’Or, Ronaldo alisema anadhani mshindi wa mwaka huu atakua Lionel Messi wa FC Barcelona.

2E5F1D4700000578-3316210-image-m-200_1447369381559

“Mimi na Messi hatuna upinzani tunamahusiano ya kawaida, tumekuwa tukiwania tuzo ya Ballon d’Or kwa pamoja kwa miaka nane lakini hakuna wengine waliowahi kufanya hivyo bali ni sisi pekee, Messi amecheza klabu moja mimi nimecheza vilabu tofauti, kiukweli tunamahusiano mazuri japokuwa sio marafiki katika maisha ya kawaida ila kila mmoja anamuheshimu mwenzake” >>> Ronaldo

“Kuhusu mama wa mtoto wangu kutojulikana kwangu mimi sioni tatizo wapo watoto wengi duniani hawana mama, Cristiano Junior anaye baba mzuri,bibi na suport kutoka katika familia yangu, naona ni sawa tu, najua watu wanajiuliza kwa nini hayupo wazi kiukweli kuna vitu katika maisha ni private na watu wanapaswa kuheshimu lakini Cristiano Junior atakapokuwa nitamwambia ukweli kuhusu mama yake ila siwezi kusema sababu watu wanataka niseme” >>> Ronaldo

“Katika akili yangu nimepanga kustaafu soka katika vilabu vya juu na vyenye ushindani na heshima kwangu lakini haina maana ya mimi kwenda kucheza Qatar, USA au Dubai sio vizuri kwangu lakini siwezi kujua ya mbele” >>> Ronaldo

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments