Michezo

Cristiano Ronaldo amekiri kuwa Benitez anazingua, kamwambia haya Rais wa Real Madrid…

on

Kwa wiki kadhaa sasa mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo amezidi kuingia katika headlines, kwa mara nyingine tena staa huyo anaingia katika headlines baada ya kutajwa kumwambia Rais wa klabu ya Real Madrid  Florentino Perez kuhusu uwezo wa kocha  wao wa sasa Rafael Benitez.

cristiano-ronaldo-593951

Cristiano Ronaldo amekuwa akitajwa kutaka kuhama klabu hiyo licha ya kuwa maneno yanayotajwa kumwambia Rais wa klabu hiyo kuwa kwa mbinu za Benitez hawawezi kutwaa Ubingwa, stori kutoka katika gazeti la kuaminika nchini Hispania El Confidencial limeandika kuwa Ronaldo alimwambia Perez kuwa kuendelea kuwa na Benitez hawatoshinda kitu. Ronaldo>>> “Kwa huyu kocha hatutoshinda kitu”

perezron

Ronaldo anatajwa kusema hivyo baada ya Real Madrid kupoteza mchezo dhidi ya Sevilla na kukubali kipigo cha goli 3-1, hata hivyo Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon alikiri kuwa Benitez alikuwa chaguo la nne kupendekezwa kupewa nafasi ya kuwa kocha wa Real Madrid baada ya Jose Mourinho, Joachim Low na Jurgen Klopp kutokuwa tayari.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.

Tupia Comments