Michezo

Cristiano Ronaldo anaisubiri rekodi hii kwa tabasamu tu, majibu yote ni mechi ya Sept 26

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo ambaye ni baba wa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Cristiano Ronaldo Junior, September 25 amepiga picha na kuiweka katika account yake ya Instagram huku akiwa na tabasamu la furaha linalotafsiriwa kuwa ni furaha yake ya kukaribia kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Real Madrid wa muda wote.

2CBEFBE300000578-0-image-a-39_1443175044026

moja kati ya picha zake alizopost Ijumaa katika account yake ya Instagram

Cristiano Ronaldo anatajwa kuwa, huenda akaingia katika rekodi ya ufungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid endapo atafanikiwa kufunga hat trick katika mchezo wa September 26 dhidi ya Malaga katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu. Rekodi ya ufungaji wa muda wote kwa sasa inashikiliwa na Raul  ambaye ana magoli 323.

2CB10F9A00000578-3248839-Ronaldo_did_not_score_as_Real_Madrid_secured_a_hard_fought_2_1_a-a-55_1443177400612

Uwezekano wa Cristiano Ronaldo kuvunja rekodi hiyo Jumamosi ya September 26 upo licha ya kuwa hadi sasa amefunga goli nane katika mashindano yote kwa msimu huu ila bado hajafunga goli lolote katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu msimu huu. Ronaldo alifunga goli tano katika mechi ya Laliga dhidi ya Espanyol na alifunga hat trick katika mechi ya UEFA dhidi ya Shakhtar Donetsk.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments