Michezo

Uamuzi wa mahakama kuhusu rufaa ya Cristiano Ronaldo huu hapa

on

FBL-ESP-LIGA-REALMADRID-MALAGAKama utakumbuka wiki mbili zilizopita mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo alitolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kujihusisha na vitendo visivyo vya kiunamichezo katika mchezo wa ligi kuu ya Spain dhidi ya Atletico Bilbao, matokeo ya kitendo kile mchezaji huyo alifungiwa mechi 3 za ligi.

Klabu yake ya Real Madrid walikataa rufaa kwenye chama cha soka na rufaa yao ikatupwa, baada ya hapo Madrid wakakata rufaa tena kwenye mahakama ya michezo nchini humo, na leo hii mapema mchana mahakama hiyo ya michezo imetoa uamuzi wake kwamba Ronaldo alistahili adhabu yake hivyo ataendelea kuitumikia.

Kwa maana hiyo mchezaji huyo ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Elche, huu ndio utakuwa mchezo wa mwisho katika kutumikia adhabu kwa Ronaldo. 

 

Tupia Comments