Michezo

Alichosema Cristiano Ronaldo baada ya kufungwa na Barcelona jana.

on

382168_heroaCristiano Ronaldo amezungumza baada ya kipigo cha jana kutoka kwa FC Barcelona akisema walikuwa wakicheza na Barca yenye wachezaji 12 yani refa wa mchezo huo Undiano Mallenco alichangia timu yake kupoteza hii mechi Santiago Bernabeu.

Madrid walipewa penati ya utata muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza lakini Mallenco aliwapa Barcelona penati mbili muda mfupi baadae na kumtoa kwa kadi nyekundu Sergio Ramos ndio maana anaamini refa aliwapendelea Barcelona kwa makusudi.

“Undiano Mallenco hafai kuchezesha michezo ya namna hii, tulikuwa tunacheza dhidi ya wachezaji 11 na mwingine wa ziada, mara zote imekuwa hivi ni kama vile hawataki tushinde ili Barcelona watetee taji la La Liga, sitafuti visingizio lakini sitaki kukaa kimya kuhusu hili, huyu refa hakustahili kuchezesha’

“Nimekuwa hapa kwa muda mrefu wa miaka mitano nafahamu mambo yanavyoenda, kama Barcelona wangepoteza hii mechi wasingekuwa na matumaini ya ubingwa tena, sijawahi kuona Madrid wakipendelewa na refa…. na pamoja na yote yaliyotokea Madrid bado tutachukua ubingwa wa La Liga”

Kama hutaki kupitwa na stori kama hizi jiunge na familia ya millardayo.com kupitia facebook twitter na instagram kwa jina hilohilo la @millardayo

Tupia Comments