Michezo

Rooney hana magoli ya kutosha, Kocha ana lolote? Mpango wake ni huu kwa Rooney..

on

Kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson amemwambia nahodha wa Timu hiyo Wayne Rooney kuwa hatasita kumuacha kwenye kikosi hicho endapo ataendelea kucheza chini ya kiwango.

Kauli hii ya Kocha Hodgson inakuja baada ya mchezaji huyo ambaye pia ni nahodha wa Manchester United kuonesha kiwango duni ambapo ameshindwa kufunga bao lolote katika mechi kadhaa mpaka sasahivi .

Rooney kwenye msimu huu amefunga jumla ya mabao manne kwenye mechi 10, sita zikiwa mechi za ligi ambako amefunga bao moja na nne za ligi ya mabingwa akiwa amefunga mabao matatu.

Kocha Roy Hodgson amesema kuwa hatasita kumuweka benchi Rooney endapo hataonyesha kiwango.

Kocha Roy Hodgson.

Katika mchezo wa juzi kwenye ligi ya mabingwa, Rooney alikosa bao la wazi baada ya kupaisha juu mpira uliopigwa na mshambuliaji Anthony Martial akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga.

Hata hivyo Rooney atakuwa na nafasi ya kucheza kwenye mechi zinazofuata za England ambapo ataweza kuizidi rekodi ya gwiji Bobby Charlton kama mfungaji bora wa miaka yote wa timu ya taifa ya England.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments