90 Day Fiance ni Kipindi ambacho kinarushwa kupitia TV iitwayo TLC (Reality TV Show) huko nchini Marekani.
Kipindi hicho ufuatilia couple ambayo imeomba K-1 Visa na hii uwa inatolewa kwa mtu ambae sio Raia wa Marekani ambae yuko kwenye mahusiano na Mmarekani.
Kwahiyo kama ukifuata masharti yao ndani ya siku 90 basi unaweza ukawa na uhalali wa kuwa na Uraia wa Marekani.
Inaelezwa K- 1 Visa inagharimu kiasi cha Dola za Marekani Elfu $ 2025 na kuipata hiyo ndio itakupa uhalalisho rasmi wa kuishi Marekani na mwenza wako.
Sasa katika msimu mpya wa pili wa kipindi cha 90 Day Fiance time hii walikuja nchini Tanzania kwaajili ya kurekodi vipindi vyao na Rosa Ree ameonekana kushiriki.
Inaonekana kwamba Wamarekani wamevutiwa sana na ushiriki wa Rosa Ree katika kipindi hicho huku wengi wakitamani aendelee kuwepo.
Unaweza ukatazama hapa alichokifanya Rosa Ree pia na kuzisoma comments za Wamarekani namna walivyomsifia na kumpongeza.
Dolla 2025