Habari za Mastaa

Rosa Ree kafungiwa kufanya muziki na faini ya millioni mbili kwa makosa haya

on

Msanii Rosa Ree amefungiwa kujihusisha na muziki kwa muda wa miezi Sita na kupigwa faini ya Millioni mbili baada ya kukutwa na makosa mawili kupitia video ya wimbo wake wa ‘vitamin U’ alioshirikiana na msanii Timmy Tdat kutokea Kenya

Mkurugenzi wa Fedha na utawala Onesmo Kayanda ambaye kwa sasa anakaimu ofisi baada ya Katibu Mkuu wa BASATA kusafiri kikazi, amesema makosa yaliyopelekea Rosa Ree kufingiwa ni mawili ambayo kwa kila kosa ameadhibiwa kulipa millioni moja na kufungiwa muziki kwa miezi 6.

“Nikweli tumemfungia kwa miezi sita kwa makosa Mawili, Kosa la kwanza ni ishu ya maadili na kosa la Pili ni kukiuka utaratibu wa Baraza ambapo amekiuka kwenda nje ya Nchi kufanya kazi bila kupata kibali kwani taratibu zipo hivi Msanii yoyote haruhusiwi kwenda nje ya nchi kufanya kazi ya Sanaa bila kibali,

“Kwahiyo sisi kama mamlaka tumemuadhibu kwa makosa Mawili na kila kosa tumemuadhibu Millioni Moja kwahiyo jumla ni Millioni Mbili na tumemfungia kazi kwa Muda wa miezi Sita lakini mtu akishahukumiwa anaweza kupima mwenyewe kama ameonewa ama ameadhibiwa sahihi na kosa lake, kwahiyo tumempa siku 30 Sheria inamruhusu kwenda kukata rufaa Kwenye waziri mwenye dhamana” – Onesmo Kayanda

 

VIDEO: MIMBA YA UWOYA: KAJIBU HAYA ALIPOULIZWA

Soma na hizi

Tupia Comments