Habari za Mastaa

Kwenye beef ya Meek Mill & Drake, Rick Ross yupo upande wa Meek Mill, kwanini? + (Video).

on

Rick Ross ameitembelea tena studio ya Power 105.1 Radio lakini safari hii ilikuwa kwa ajili ya interview na mmoja kati ya presenters wakubwa wa radio Marekani, Angie Martinez

RICKI4

Angie Martinez wa Power 105.1 Radio Marekani.

Kwenye interview hiyo Rick Ross ameongelea beef kati ya Meek Mill na Drake na kusema kuwa haoni kama beef hiyo imemuathiri Mee Mill kwa vyovyote vile huku akisifu nyimbo za Meek kuwa ni kali mno! kwa kiasi kikubwa sana inaonekana Rick Ross yupo upande wa Meek Mill… kwanini?

RICKI3

Rick Ross.

Akiwa kwenye interview hiyo Rick Ross alisema haya kuhusu beef ya Meek Mill na Drake

>>> “Watu siku zote wanakuwa na mitazamo tofauti, ndio maana inaitwa mitazamo, na siku zote mitazamo haifanani na wala haimaanishi kuwa mitazamo hiyo inamaanisha chochote, hata mimi mwanzoni walisema mimi sio mkali na siwezi kukaa kwenye game muda mrefu.. lakini leo!?<<< Rick Ross.

RICKI2

Rapper huyo hakuishia hapo, aliendelea kusema kwanini Meek Mill atakua zaidi kimuziki baada ya haya kutokea…

>>> “Meek Mill atashine zaidi baada ya hapa, wala hatakufa kimuziki nalikataa hili kabisa kwasababu hivi ndio vitu vinavyokujenga kimuziki, kama hawakushambulii basi huwezi kukua hii inaonyesha kuwa ana kitu… huwa pia namshauri Meek Mill, namwambia aendelee kutengeneza muziki na afanye kitu pale tu anapoona yupo tayari kufanya kitu hicho, na kama watu wamechukulia hii beef serious basi.” <<< Rick Ross.

RICKI

Badaae Rick Ross akaulizwa kuhusu mtazamo wake wa nyimbo za Meek Mill, rapper huyo alikuwa na haya ya kusema…

>>> “Nyimbo za Meek Mill ni kali sana, dogo anajua… mpaka sasa nina nyimbo 6 mpya za Meek Mill kwenye simu yangu na zote ni hit songs, zote sita!” <<< Rick Ross.

Unawez ukamsikiliza Rick Ross mwenyewe kwenye hii video hapa chini mtu wangu.

https://youtu.be/U-O0lOR5ux4

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM, TWITTER, FB, YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments