Habari za Mastaa

Rick Ross na mpenzi wake Lira Galore kuvunja uchumba..!? Sababu?

on

CEO wa lebo ya Maybach Music Group (MMG) Rick Ross ameingia kwenye headlines za burudani baada ya mtandao wa TMZ Marekani kuripoti kuwa mapenzi na mahaba kati ya rapper huyo na mchumba wake Lira Galore yapo matatani kuisha!

Imepita miezi miwili tu toka Rick Ross aweke headlines nyingi sana kwenye social networks na websites baada ya kutangaza kuwa amemvesha pete ya uchumba mpenzi wake Lira Galore na very soon wawili hao watakula kiapo cha kuishi milele kama wanandoa… hali leo ipoje?!

ROSSAY2

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, wawili hao wameingia kwenye majibishano makubwa kitendo kilichopelekea Lira kuamua kupaki vitu vyake na kuhama kwenye nyumba ya Rick Ross, japo chanzo cha ugomvi wao bado hakijaweka hadharani ila Rossay ameonekana kukubaliana na kitendo hicho na kusita kuongea kitu chochote kwa sasa huku baadhi ya mitandao Marekani ikiripoti kuwa kuvunjwa kwa engagement hiyo ni kutokana na Lira kukutwa na mtu mwengine!

ROSSAY3

Baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa, Rick Ross alifanya maamuzi ya kumvesha mpenzi wake pete ya uchumba yenye thamani zaidi ya milion 700 za Kitanzania katikati ya mwezi September mwaka 2015 baada ya wawili hao kuchagua pete hiyo kwenye duka la pete jijini New York.

ROSSAY2

Pete ya uchumba aliyovalishwa Lira Galore na Rick Ross.

Lakini kabla ya kutengana dada huyo alipata shavu la kuonekana kwenye video mpya ya Rick Ross ” Sorry Video” na pia kuonekana na rapper huyo kwenye tuzo za BET Hip-Hop Awards mwezi mmoja uliopita, isitohe mwaka 2012 Lira alishawahi kujitabiria kupitia page yake ya Twitter kuwa atakuja kufunga pingu za maisha na rapper huyo lakini kwa muonekano wa mambo sasa hivi inaonekana kama ndoto hizo zinaweza kuishia njiani.

ROSSAY3

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments