Top Stories

Familia za Kifalme zinazoongoza kwa Utajiri Barani Ulaya

on

familia ya kifalme ya uingereza

Katika Mataifa yenye utamaduni wa kuongozwa na familia za kifalme au malkia Utawala wa Malkia Elizabeth wa Uingereza ndio maarufu kuliko familia zote zinazoongoza.

Japo familia hii ni maarufu lakini sio tajiri kama ambavyo watu wanaweza kudhani wakilinganisha umaarufu na ukubwa wa nchi anayoiongoza, Malkia Elizabeth na uwezo wa kifedha.

Familia ya kifalme inayoongoza taifa la Lichtenstein ndio inayoongoza kwa utajiri ikiwa na utajiri wa paundi bilioni 4.9.

Ikiongozwa na Prince Hans-Adam II, familia hii ina utajiri ambao hauna uhusiano wowote na kodi za wananchi wa taifa dogo la Lichtenstein na utajiri walio nao kina Hans-Adam II unatokana na kampuni ya LGT Holdings ambayo inajiendesha kwa faida kubwa tofauti na familia nyingine za kifalme ambazo zina utajiri unaotokana kwa kiasi kubwa na kodi za wananchi wao.

Prince Hans-Adam II ndiye kiongozi wa kifalme tajiri kuliko wote barani ulaya .

Prince Hans-Adam II ndiye kiongozi wa kifalme tajiri kuliko wote barani ulaya.

Familia ya Kifalme ya Monaco inayoongozwa na Prince Albert II inashika nafasi ya pili kwa wafalme na Malkia wa Ulaya ambapo ina utajiri wa paundi bilioni 1 wakiwa wanaendesha biashara ya makazi kwenye eneo la  Monaco ambalo ni moja ya mataifa madogo kuliko yote duniani.

Familia ya Malkia Elizabeth ambayo inafahamika kama familia ya Windsors yenyewe ina utajiri wa paundi milioni 295 ikiwa inaongoza mataifa ya Uingereza na visiwa vyake vinne, Canada, Australia, New Zealand na maeneo mengine ya Jumuiya ya Madola.

Malikia Elizabeth na familia yake wana utajiri wa paundi milioni 293.

Malkia Elizabeth na familia yake wana utajiri wa paundi milioni 295.

Familia ya kifalme ya Uholanzi inayofahamika kama Orange-Nassau inashika nafasi ya nne kwenye orodha ya familia za kifalme zenye utajiri . Familia hii ina utajiri unaokadiriwa kufikia paundi milioni 131 ambao kwa kiasi kikubwa unatokana na biashara binafsi zikiwemo kampuni ya mafuta ya Shell.

Utajiri wa familia hii ya kfialme ya Uholanzi unadhaniwa kuwa mkubwa zaidi ya makadirio haya kutokana na ukweli kuwa haujawahi kutamka wazi kiasi cha fedha kinachomilikiwa na familia hii.

Familia ya Bernadotte ya Sweden ambayo inaongozwa na Mfalme Carl Gustaf XVI inashika nafasi ya tano nyuma ya familia inayoongoza Uholanzi.

Familia ya kifalme ya Hispania ni moja kati ya familia zenye utajiri mdogo japo inamiliki kasri kubwa kuliko zote za kifalme duniani .

Familia ya kifalme ya Hispania ni moja kati ya familia zenye utajiri mdogo japo inamiliki kasri kubwa kuliko zote za kifalme duniani.

Familia hii inautajiri wa paundi milioni 27.5

Mfalme wa Norway, Harald V ndiye kiongozi mwenye utajiri kiduchu kuliko wote akiwa na kiasi cha Paundi milioni 12 pekee.

Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments