beef

Beef: 50 Cent na Rick Ross wafufua beef yenye miaka zaidi ya mitano kwenye mitandao ya kijamii!

on

Wasanii wa muziiki wa HipHop Marekani, 50 Cent na Rick Ross wanaziandika headlines baada ya wawili hao kufufua beef ya mwaka 2009 kati yao kwenye social media… ugomvi ulianza siku ya ijumaa baada ya 50 Cent kupost picha kwenye Instagram T-shirt ya kumkejeli Rick Ross na maneno yaliyosema ” Lmao ???? sina cha kufanya kwa hiyo nimeamua kuuza hizi Tshirt kwa $2.95″.

ROSSAY50

Baada ya dakika kadhaa 50 alifuta post hiyo lakini Rick Ross alikuwa ameshakutana nayo, Rozay akaamua kumjibu 50 kupitia page yake ya Twitter, akaandika tweet ya kumshambulia 50 Cent iliyosema; “Forced into #BANKRUPTCY now the Donkey @50cent WORKING 4 #MMG Merch co. selling T’s for 2.95 on the #BLACKMARKET haaa!” 

ROSSAY502

Majibizano yao kupita Instagram na Twitter hayakuishia hapo, 50 Cent alirudi tena kwenye Instagram na kuendelea kumshambulia Boss wa Maybach Music Group, Rick Ross kwa kupost picha ya kitambo sana ya Rozay kipindi hicho akiwa Askari Magereza na kumtania kuhusu engagement yake kwa mchumba wake Lisa Galore mwenye miaka 22… kwenye post hiyo 50 aliandika;

>>>” Ok hii movie ni kali ???? askari magereza anayerap kama mvuta bangi mpaka anajiamini kuwa ni hivyo, kisha anajishaua sana alafu mauzo yake kimuziki sio kitu kikubwa na badaae anaamua kumchumbia stripper wa miaka 22 ambaye kwa asilimia kubwa crew yake nzima imeshampitia…LMAO ☕️???? subiri kwanza, ningependa kununua hakimiliki juu ya hii movie”. <<< @50cent.

ROSSAY50350 Cent hakuishia hapo akaamua apost tena picha nyingine ya Ricky Rozay, lakini hii ililenga ile beef kati ya msanii wake Meek Mill na msanii kutoka Cash Money Records, Drake… huku caption yake ikisema;

>>> ” Hivi ndiyo unavyokuwa… pale ambapo DRAKE ALIMKALISHA MTU WAKO. LMAO hii ndio emoji mpya ya MMG ???? kuangalia lakini husemi kitu… ” <<< @50cent.

ROSSAY504

Rick Ross naye akaendelea kumshambulia 50, sema round hii Rozay alimshambulia 50 cent na mwanae kupitia page yake ya Twitter na Instagram, Rick Ross alipost na kutweet;

ROSSAY506

ROSSAY507

Beef kati ya Rick Ross na 50 Cent ilianza mwaka 2009 ambapo 50 alivujisha mkanda wa utupu wa aliyekuwa mpenzi wa Rick Ross wakati ule Lastonia Leviston, japo 50 cent alidai kuwa si yeye aliyehusika kwenye kuvujisha mkanda huo Lastonia aliamua kwenda kushitaki Mahakamani ambapo badaae kulitokea mvutano mkubwa sana kati ya watu hao watatu.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments