Habari za Mastaa

Mapenzi yanaendelea kati ya Rick Ross na mchumba wake kwenye hii mpya ‘Sorry’ feat. Chris Brown – (Video)!

on

Kumekuwa na maneno mengi sana juu ya Rick Ross na mchumba wake Lira Galore, mitandao mingi ya Marekani iliripoti kuwa wawili hao wameachana na kuwa Rozzay kavunja uchumba na mwanamke wake baada ya kumkuta na mwanaume mwengine.

Lakini kwenye video mpya ya Rick Ross feat Chris Brown, Sorry inaweza ikakupa picha nyingine kabisa kuhusu maneno yote amabayo unaweza ukawa umeyasikia kuhusu boss wa Maybach Music Group na fiance wake Lira Galore… wimbo huu mpya pia unapatikana kwenye Album mpya ya Rick Ross, Black Market inayotegemea kuwa mtaani tarehe 4 December 2015.

ROZE

Video mpya ya Ricky Rozzay  feat Chris Brown ipo hapa chini, ukibonyeza play unaweza kuicheki moja kwa moja.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

 

Soma na hizi

Tupia Comments