Leo May 1, 2018 Ripota wa BBC ameuawa katika shambulio lililotokea huko Mashariki mwa Afghanistan katika Jimbo la Khost.
Ahmad Shah, aliyekuwa na miaka 29, amefanya kazi na BBC Afghan kwa zaidi ya mwaka sasa.
Katika taarifa aliyoitoa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la BBC duniani, Jamie Angus amesema Shah alikuwa ni mtu mwenye “kuheshimika na maarufu” katika kazi yake ya uandishi wa habari.
“Tumepoteza mtu muhimu na ninatuma salamu zangu za rambirambi kwa familia ya Ahmad Shah na rafiki zake pamoja na timu nzima ya Shirika la Habari la BBC huko Afghan,” amesema kiongozi huyo.
“Tunafanya kila kinachowezekana kuisaidia familia yake wakati huu mgumu.”
Mkuu wa Polisi wa Jimbo la Khost, Abdul Hanan ameieleza BBC Afghan kuwa Shah alipigwa risasi na watu waliokuwa na silaha ambao hawajafahamika. Amesema, Polisi bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na sababu za kuuawa kwake.
Wenyeji walioshuhudia wameieleza BBC kuwa, Shah alikuwa katika baiskeli yake wakati tukio hilo linamtokea. Alichukuliwa na wenyeji na kukimbizwa hospitalini ambapo alifariki duniani kutokana na majereha.
MAGAZETI LIVE: Mabilioni yayeyuka, Lissu Nimesahau kutembea, Kigezo kipya Mikopo Vyuo Vikuu