Top Stories

Staa wa Rugby alivyong’atwa na simba kwa ‘ujinga’

on

Mchezaji wa Rugby wa timu ya Welsh international ya Uingereza Scott Balwin amejikuta ameraruriwa na simba mkononi baada ya kujaribu kumchezea simba huyo kichwani kama mnyama wa kawaida wa kufugwa akiwa kwenye ziara na timu yake kwenye hifadhi ya wanyama ya Bloemfontein huko Afrika Kusini.

Inaelezwa kuwa wakati timu hiyo inawasili kwenye hifadhi hiyo walipewa onyo la kutoingiza mikono kwenye vyumba hivyo ambavyo wako simba au wnyama wengine kwani ni hatari na kitendo cha Scott kukiuka maelekezo hayo kimetafsiriwa kuwa ni ujinga.

Boss wa Scott aitwaye Steve Tandy ameeleza kuwa hali yake inaendelea vizuri na ameshonwa yuzi kadhaa lakini amkitishwa na alichofanya mchezaji huyo na kusema kuwa hicho kilikua kitendo cha kijinga cha yeye kufikiri anaweza kumchezea simba kama anavyomchezea paka wa nyumbani ikiwa walishapewa maelekezo wakati wanaanza ziara yao.

Ulipitwa? FIESTA MWANZA 2017: Alikiba LIVE na shangwe la ‘mwana’

Soma na hizi

Tupia Comments