Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi ajira,vijana na watu wenye Ulemavu Professa Joyce Ndalichako ametembelea mradi wa machinjio ya kisasa cha Nguru Hills Ranch kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.
KIWANDA CHA NYAMA NGURU HILLS RANCH CHAANZA UZALISHAJI ,NYAMA KUUZWA UARABUNI.
Profesa Ndalichako ameriidhika na maendeleo ya kiwanda hicho kwani kwa sasa kipo katika hatua ya majaribio kwa kipindi cha miezi mitatu ili kujaribu mitambo pamoja na ununuzi wa malighafi.
Profesa Ndalichako amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia imedhamiria kuwekeza katika viwanda hivyo upatikanaji wa kiwanda hicho ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Fourtunatus Magambo ni mkurugenzi uwekezaji PSSSF amesema kiwanda hicho kwa sasa kinauwezo wa kuchinja Ng”ombe 100 na Mbuzi 1000 kwa siku moja jambo ambalo linatajwa kuwa mwarobaini wa changamoto ya wakulima na wafugaji wilayani Mvomero na mkoa Morogoro kwa ujumla
Mgambo amesema mifugo inayochinjwa katika kiwanda hicho inanunulia sehemu mbalimbali nchini na kwa kuzingatia vigezo maalum ikiwemo uzito usipongua kilo 250 kwa ng”ombe mmoja.
Amesema baada ya kununua mifugo inapumzishwa kwa kipindi cha miezi mitatu ndipo inachinjwa ili kuongeza uzito
Amesema eneo la kiwanda ni kubwa linauwezo wa kuhifadhi ngombe 1000 na mbuzi 1500 kwa pamoja kabla ya kuingia katika machinjio.
Aidha amesema nyama inayozalisha katika mkiwanda hicho kwa asilimi 80 nyama itauzwa nchi za uarabuni ambako kutakua na soko kubwa huku asilimia 20 ikiuzwa hapa nchini.
Amesema kiwanda kinauwezo wa kuajiri wafanyakazi zaidi ya mia tatu ajira za kudumu na 2000 ajira za muda.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Halima Okash amesema uwepo wa kiwanda hicho ni fursa kwa vijana pamoja na wafugaji hivyo atahakikisha anahamasha wafugaji kuuza mifugo yako katika kiwanda.
Okash anasema licha ya vijana kupata ajira lakini atahakikisha anasimamia mapato yanayopatikana katika kiwanda hicho.