Rubani wa zamani wa Marekani amepokea tuzo ya juu zaidi ya kijeshi nchini humo kwa kukataa kutekeleza maagizo ya moja kwa moja ya kijeshi wakati wa Vita vya Vietnam.
Rais wa Marekani Joe Biden alimtunuku Nishani ya Heshima katika Ikulu ya White House rubani mstaafu Larry Taylor, ambaye sasa ana umri wa miaka 81, ambaye alikuwa ametumia helikopta yake ya Cobra katika mapigano ya bunduki ili kuokoa wanajeshi wanne wa Marekani kutokana na kifo mwaka 1968.
Amri hiyo ilimtaka Taylor aondoke kwenye vita na kurejea katika kituo chake, lakini alikataa na kuamua kujihusisha na kuwaokoa wanajeshi wa Marekani alipojua kwamba hakuna helikopta nyingine ya uokoaji iliyotumwa.
Jeshi linasema kuwa helikopta za Cobra hazijawahi kutumika katika kazi ya uokoaji ya askari, kwa vile ni helikopta ya mashambulizi na haina uwezo wa kusafirisha askari.
Kwa sababu helikopta ya Cobra inaweza kubeba watu wawili tu, askari walilazimika kung’ang’ania nje na kutoroka kutoka eneo la mashambulizi.
“Haikuwezekana kutuma helikopta ya uokoaji,” Rais Biden alisema katika hafla ya kukabidhi nishani siku ya Jumanne. “Badala yake, Luteni Taylor alipokea amri ya moja kwa moja: kurudi kwenye kituo. Jibu lake lilikuwa la moja kwa moja: ‘Ninawatoa watu wangu.’
Article share tools