Gazeti la Daily Mail linamtaja Ruben Amorim wa Sporting Lisbon kama mgombea wakuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino huko Stamford Bridge.
Pochettino amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, na mwaka mwingine kama chaguo ikiwa klabu itataka kuuchukua.
The Mail linaandika: “Nafasi ya muda mrefu ya kocha mkuu wa Chelsea, Mauricio Pochettino, kama kocha mkuu haina uhakika, huku kufuzu kwa soka la Ulaya kukiibuka kuwa jambo muhimu katika kuamua mustakabali wa Muargentina huyo.
“Presha inazidi kupanda kwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 kufuatia timu yake kupoteza fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Wembley siku ya Jumapili.
Pochettino alisaini mkataba wa miaka miwili msimu uliopita wa joto, na chaguo la tatu.
Chelsea wana nia ya muda mrefu ya kumnunua Ruben Amorim katika klabu ya Sporting Lisbon, lakini Mreno huyo anatarajiwa kuwa na chaguzi za hali ya juu ambao wanaweza kumpa soka la Ulaya msimu ujao.”