AyoTV

VIDEO: Imenifikia ripoti ya tuhuma za rushwa Tanzania, Waziri mkuu hajaikalia kimya..

on

Headline juu ya headline zimeendelea kutawala ndani ya Bunge la Tanzania, na leo April 22 2016 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipata time ya kulihutubia Taifa. Hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2016/2017

Waziri Majaliwa ameyazungumza haya……..>>>’Serikali imeendelea kupambana na tuhuma za rushwa na kuwafikisha watuhumiwa mbele ya vyombo vya sheria.

>>>’Katika mwaka 2015/2016, Serikali imeshughulikia tuhuma 3,911 ambapo uchunguzi wa tuhuma 324 ulikamilika. Serikali itaendelea kuchunguza tuhuma 3,444 zilizopo na mpya zitakazojitokeza na kukamilisha uchunguzi wa tuhuma 10 za rushwa kubwa.

>>’Aidha tutawajengea uelewa wa masuala ya rushwa makundi mbalimbali katika jamii na hususani asasi za kiraia, madhehebu ya dini na wanahabari

Baada ya kueleza yote, Waziri Mkuu Majaliwa akatumia nafasi hiyo kutangaza makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri mkuu kwa mwaka 2016/2017

 ambapo amesema>>> ‘Kwa mwaka 2016/2017, Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake inaliomba Bunge liidhinishe jumla ya Shilingi 236,759,874,706. Kati ya hizo, Shilingi 71,564,293,773 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi 165,195,580,933 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo

ULIIKOSA YA DIAMOND, MRISHO MPOTO WALIVYOTAJWA BUNGENI?ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments