Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF Mwita Waisaka leo ametoa majibu ya marejeo ya adhabu ya mjumbe wa DRFA Shaffih Dauda ya kufungiwa miaka mitano kujihusisha na soka.
Maamuzi ya Kamati ni kuwa Shaffih Dauda ataendelea kutumikia adhabu yake kama kawaida kutokana na Shaffih Dauda kutohudhuria siku iliyopangwa ya kufanya marejeo.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri February 16 2022 Shaffih Dauda alifungiwa miaka mitano na faini ya Tsh milioni 6 kutokana na chapisho lake la mitandao ya kijamii ambalo lilikuwa linaituhumu TFF.
Marejeo ya adhabu ya Shaffih Dauda yamefanyika baada ya BMT kuzuia DRFA kufanya uchaguzi jana katika Mkutano Mkuu wake kujaza nafasi ya Shaffih Dauda kutokana na kuwa hakukuwa kumefanyika marejeo ya hukumu yake kama alivyoomba.