Rufaa ya usma Algeir dhidi ya Ushindi waliopewa Rs Berkane imetupiliwa mbali na mahakama maalum ya rufaa za michezo CAS baada ya kuonekana hakuna hoja ya msingi.
Itakumbukwa kuwa Berkane walipewa ushindi baada ya Usma kuwagomea kucheza na jezi zao za kawaida kufuatia mzozo wa kidiplomasia unaoendelea kati ya Morocco na Algeria chanzo kikiwa harakati za ukombozi wa ukanda wa Sahara Magharibi.
Usma waliomba mchezo wao dhidi ya Berkane urudiwe huku matokeo ya ushindi waliopewa waMorocco ukifutwa jambo ambalo CAS imelikataa.
Cas inayatambua rasmi matokeo ya mwisho yaliyowapa ushindi Berkane ambao walifuzu fainali na kufunga rasmi mjadala wa mzozo wa jezi uliojitokeza msimu uliopita.
Hapakuwa na adhabu yoyote dhidi ya Rs Berkane kwenye hukumu iliyosomwa dhidi ya Rufaa ya Usma.