Top Stories

Rugemalila aachiwa Huru, DPP amefuta mashtaka

on

Baada ya kusota mahabusu kwa takribani miaka 4, Hatimaye aliyekuwa Mkurugenzi wa IPTL, mfanyabiashara James Rugemalira ameachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Rugemalira alifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 19, 2017 pamoja na wenzake wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2027 yenye mashtaka 12.

Mashtaka ya Rugemalira yameondolewa chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwanendo wa Makosa ya Jinai, DDP amefuta mashtaka hayo na yeye kuachiwa huru.

Miongoni mwa mashitaka yanayowakabili wanadaiwa kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19,2014 jijini Dar es Salaam, walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India kwa ajili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Katika shitàka la pili la kujihusisha na mtandao, washtakiwa hao kati ya Oktoba 18,2011 na Machi 19,2014 jijini Dar es Salaam wakiwa sio watumishi wa umma walitekeleza mtandao huo wa uharibifu kwa lengo la kujipatia faida.

Katika shtaka la tatu, Sethi anadaiwa Oktoba 10, 2011, katika mtaa wa Ohio Ilala Dar es Salaam, akiwa ana nia ya ulaghai alighushi fomu namba 14 ya usajili ya kampuni na kuonyesha yeye ni Mtanzania anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua ni uongo.

TUNDU LISSU AFUNGUKA UTARATIBU MPYA WA USIKILIZWAJI WA KESI YA MBOWE “HAKI LAZIMA IFANYIKE”

KESI YA MBOWE NA WENZAKE BADO HAIJAANZA, WAFUASI WA CHADEMA WAZUILIWA KUINGIA MAHAKAMANI

Soma na hizi

Tupia Comments