Habari za Mastaa

Runtown na Dj Khaled kwenye Album moja?! + mastaa wengine waliowahi kutoa nyimbo na Wamarekani!

on

Siku hizi biashara ya muziki Africa imekuwa ya ushindani mkubwa sana, wasanii wamewekeza juhudi, muda na hela kubwa kwenye kutengeneza muziki sio tu wa Africa bali muziki utakaopokelewa na dunia nzima kwa ujumla.

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Runtown anaongeza idadi ya wasanii kutoka Africa ambao wameaonyesha uthubutu kwa kuwashirikisha wasanii wenye majina makubwa kwenye Industry ya Muziki baada ya kumshirikisha Proucer, Mtangazaji na Dj maarufu kutoka Marekani, Dj Khaled kwenye moja ya nyimbo zilizopo kwenye album yake mpya!

RUNKHALED4

Kupitia page yake ya Instagram, Runtown ameachia orodha ya nyimbo zitakazokuwepo kwenye Album yake mpya ‘Ghetto Unievesity’ itakayokuwa sokoni rasmi siku ya Jumatatu tarehe 23 November 2015 yani wiki mbili kuanzia sasa.

RUNKHALED4

Ukiacha mbali kufanya kazi na Dj Khaled, wasanii wengine walioshirikishwa kwenye Album hiyo ni pamoja na Wizkid, Davido, Uhuru na Dj Maphosira kutoka South Africa, MI Abaga na wengine.

RUNKHALED3

Runtown alikuepo nchini mwezi uliopita kwa ajili ya finali za Bongo Star Search 2015 na alithibitisha kufanya kazi na msanii wa Tanzania kutoka kwenye kundi la TMK Wanaume Family, Chege Chigunda.

RUNCHEGE

Hapa chini nina orodha kamili ya nyimbo zitakazo kuwepo kwenye Album hiyo…

Money Bag ft. DJ Khaled
Let me love You
Gallardo ft. Davido
The Banger ft. Uhuru
Kilofoshi
Talk for me
Ima  Ndi Anyi Bu ft. Phyno
Omalicha Nwa
Tuwo Shinkafa ft. Barbapappa
Ghetto University
Bend Down Pause ft. Wizkid
Walahi
Lagos to Kampala ft. Wizkid
My Guyz ft. Anatii
Sarki Zaki ft. M.I X Hafeez
Tuwo Shinkafa (Moroccan Version)
Na So the Story Go

Wasanii wengine wa Africa walioingia studio na kupiga collabo na wasanii wakubwa wa Marekani ni pamoja na mtu wetu A.Y aliyefanya ngoma na mtoto wa Producer Master P, Romeo (Lil Romeo) na Lamyia, nyingine ilikuwa na mmoja ya wakali wa dancehall kutoka Jamaica, Sean Kingston, Davido na Meek Mill, Sakodie na Ace Hood, P Square na Rick Ross, nyingine na T.I na nyingine pia na Akon, MC Galaxy na Swizz Beatz, lakini pia kwenye list yangu siwezi kuisahau ya D’banj na Akon Mkurugenzi wa Konvict Muzik.

 

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments