Stori Kubwa

Maamuzi ya jeshi la Polisi baada ya huyu Askari wa Tanga aliyenaswa kwenye video

on

Novemba 9, 2015 kulikuwa na headlines kwenye mitandao mbalimbali baada ya video kusambazwa na wasiojulikana ikimuonyesha Askari wa usalama wa barabarani Anthony Temu kutoka kituo cha polisi Kabuku Tanga akichukua rushwa kutoka kwenye gari alilolisimamisha.

Baada ya hii taarifa kusambazwa mitandaoni kamanda wa polisi mkoani Tanga, Zuberi Mwombeji amethibitisha hii ishu nzima kutokea na kwamba Temu alihojiwa na kukiri kwamba ni kweli alifanya hivyo, baada ya hapo Kamanda Mwombeji amesema wamemkabidhi kwa TAKUKURU.

Tanga 2

Moja ya picha kutoka kwenye hiyo video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Tumechunguza taarifa zile na tumemtafuta tumemshughulikia na kumkabidhi kwa maafisa wa TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi sababu wao ndio wanashughulika na maswala haya ya rushwa‘ – Kamanda Mwombeji.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments