Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa Kenya uliofanyika jana, yanaonyesha mgombea wa Kenya Kwanza na Naibu Rais, William Ruto anaongoza kwa kuwa na asilimia 50.85 huku mpinzani wake wa karibu Raila Odinga wa Azimio La Umoja akiwa na asilimia 48.52.
Ingawa bado Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya
(IEBC) haijatangaza matokeo ya jumla, Ruto amendelea kuwa kileleni akiwa na kura 680,535 dhidi ya kura 649,769 za Odinga.
•Matokeo hayo yameonyesha mchuano mkali huku IEBC ikionyesha kuwa asilimia 91 ya matokeo kutoka katika vituo yalishawafikia na kuyatangaza.
Kutokana na matokeo hayo baadhi ya wafuasi wa Ruto wamekuwa wakiingia mtaani kushangilia ushindi huku wakidai hakuna uwezekano wa Odinga kupindua matokeo na kupata ushindi.