Zaidi ya magari 5,000 aina ya Toyota yatashiriki kwenye Tamasha kubwa la Utalii mkoani Ruvuma (Ruvuma Toyota Festive) litakalofanyika tarehe 25 Juni 2025.
Aidha Tamasha hili linatarajia kuwakutanisha watu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini na nje ya Nchi.
Maandamano ya Magari aina ya Toyota yataanzia katika Manispaa ya Songea na kumalizika katika mji mdogo wa Mbambabay wilaya ya Nyasa ambalo linalenga kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo mbalimbali mkoani Ruvuma.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Peres Magiri wakati anazindua Toyota Networking Cocktail kwenye ukumbi wa kanisa Anglikana mjini Songea