Rwanda siku ya Jumapili, itaanza maadhimisho ya kitaifa ya miaka 30 kukumbuka mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya laki nane kwa kipindi cha siku 100 wengi wakiwa Watutsi.
Katika kipindi hiki Wanyarwanda wanaomboleza familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza maisha yao kutokana na maujai ya kimbari yaliyofanyika mwaka 1994 nchini Rwanda.
Kumbukizi ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda inaanza rasmi tarehe 7 Aprili na itafikia kilele chake tarehe 13 mwezi huu ambapo bendera zitashushwa nusu mlingoti katika kipindi cha wiki nzima.