Janga la Covid-19 lilidhihirisha utegemezi mkubwa wa afrika katika uagizaji wa chanjo kutoka nje ambapo kwa mujibu wa kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa CDC, ilisema chini ya asilimia 50 ya watu bilioni 1.2 barani Afrika wamechanjwa kikamilifu dhidi ya Covid-19.
Shehena ya kwanza iliyobeba vifaa vya kutengeneza chanjo kutoka kampuni ya Ujerumani ya BioNTech vimewasili nchini Rwanda jana Jumatatu, Afrika ikijitahidi kuimarisha uwezo wake wa kuzalisha chanjo.
Vifaa hivyo, vilivyotengenezwa kwa makontena yaliyochakatwa viliwasili katika mji mkuu wa Kigali, ambapo vitakusanywa ili kutengeneza kiwanda cha uzalishaji wa chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Kiwanda hicho cha mjini Kigali kitakuwa na uwezo wa kuzalisha hadi chanjo milioni 100 za mRNA kwa mwaka na kitachukua angalau miezi 12 kabla ya kuanza kutoa dozi.
Rwanda ndiyo imeandaa maabara ya kwanza ya uzalishaji wa chanjo ya simu ya BioNTech barani Afrika.
Mradi huu, unaoendelea tangu Oktoba 2021, ambao Rwanda ni mfaidika wa kwanza, unapaswa pia kuzinduliwa nchini Senegal na Afrika Kusini.
Maabara hii inayotembea ina uwezo wa kuzalisha dozi milioni 50 hadi 100 kwa mwaka.