Watu zaidi ya 127 wamepoteza maisha nchini Rwanda, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo, Magharibi na Kaskazini mwa nchi hiyo.
“Kumenyesha mvua kubwa, kuna mito ambao kingo zilivunjika na kukawa na maporomoko ya udongo ambayo yalisababisha maafa makubwa.” amesema Emmanuel Mazimpaka Afisa wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Rwanda.
Haya yanajiri wakati huu pia serikali ya Rwanda ikisema kuwa juhudi za kuwatafuta watu waliopotea na pia kuwaokoa walio hai zinaendelea baada ya kutokea mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo, Magharibi na Kaskazini mwa nchi hiyo ambapo watu mia moja ishirini na saba kupoteza.
“Kuna mto uliovunja kingo zake kutokana na mvua kubwa na maji yakateremka hadi kwenye barabara yenye lami, mimi naliita tukio hili kama janga la asilia.” ameeleza Alain Mukuralinda naibu msemaji wa Serikali ya Kigali .
Mamlaka katika maeneo husika zinasema kuwa huenda idadi ya waliofariki ikiongezeka kutokana maporomoko ya udongo yanyotokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.
Hali kama hii pia inashuhudiwa katika nchi jirani ya Uganda, ambapo watu sita wamepoteza maisha katika Wilaya ya Kisoro baada ya kusombwa na maji ya mafuriko kwa mujibu wa Shirika la msalaba mwekundu