Taasisi ya Chanjo ya Sabin imetoa takriban dozi 1,000 za chanjo kwa Rwanda, ili kuongeza juhudi za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg.
Hii ni takriban siku 10 kufuatia taasisi hiyo kutoa dozi 700 za chanjo, siku chache baada ya mlipuko wa homa ya Marburg kuthibitishwa nchini Rwanda.
Oktoba 6, mamlaka ya afya ya Rwanda ilianza kutoa chanjo kwa wahudumu wa afya walio mstari wa mbele ikiwa ni sehemu ya majaribio ya awamu ya pili ya kukabiliana na ugonjwa huo. Hadi kufikia Jumamosi, dozi 620 za chanjo zilikuwa zimetolewa.
Utoaji wa chanjo hiyo unasimamiwa kwa mujibu wa itifaki ambayo imepitiwa na kuidhinishwa na mamlaka za Rwanda.