fB insta twitter

Ray C kapost kwa mara ya kwanza tangu apelekwe kwenye matibabu Bagamoyo

on

Usiku wa June 16 2016 kuamkia June 17 kuna video ya mwimbaji wa longtime Bongoflevani Rehema Chalamila au Ray C ilisambaa mitandaoni akiwa anachukuliwa na gari la Polisi Kinondoni Dar es salaam ambapo baadae ilikuja kugundulika alipelekwa Hospitali.

Kesho yake mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba alionge na Amplifaya ya CloudsFM pamoja na millardayo.com na kuthibitisha kwamba mwimbaji huyu amekubali mwenyewe kwa hiari yake na kupelekwa kwenye nyumba ya matibabu ya kuachana na dawa za kulevya huko Bagamoyo Pwani.

Baada ya hapo tuliona ukimya sana kwenye mitandao ya kijamii na Ray C hakuwa anapost chochote tofauti na tulivyozoea alikua mtu wa kupost na hata kuongea mara kwa mara.

Leo August 3 2016 amepost maandishi yasemayo >>> ‘Sala ya amani, Mungu amenipa amani, amenipa nguvu ya kubadilisha vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wangu na hekima ya kujua utofauti, kuishi siku moja baada ya nyingine, kufurahia mda mmoja baada ya mwingine, kukubaliana na ugumu kama njia ya kukupa amani’

Picha nyingine aliyoiweka ilisema ‘KUPONA HUJA KWANZA, bili zitalipwa, kazi yako utamaliziwa, orodha itafanyika na utalipa kodi, bado familia yako itakupenda, maisha yako ya upendo yatachanua pale yakiwa tayari, utakuwa na vitu uvipendavyo, fanya moyo wako, afya yako, na msimamo wako kuwa juu ya vitu hivyo, KUPONA HUJA KWANZA’

ray c

ULIYAKOSA MAMBO TISA YA RAY C BAADA YA KUCHUKULIWA NA POLISI DSM BAADA YA KUTAKA KUJIUA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

ULIKOSA KTAZAMA VIDEO YA MUONEKANO WA CHID BENZ BAADA YA KUTOKA SOBER HOUSE? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments