Habari za Mastaa

Rayvanny aeleza furaha kutajwa kuwania MTV MAMA 2016

on

Ni mwimbaji mwingine staa wa bongofleva, makofi mengi amepigiwa kwenye utunzi pamoja na ukali wa melody, anaitwa Rayvanny kutoka WCB ambaye ngoma yake ya kwanza kuiachia toka yuko chini ya lebo ya WCB aliiachia ‘kwetu‘ April 2016.

Anazo sifa nyingine za uchapakazi pia na ndio maana leo anafurahia mafanikio/hatua yake kwa kipindi hiko kifupi ambapo October 3, 2016 alitajwa kuwania tuzo kubwa za MTV MAMA 2016 katika kipengele cha Best Breakthrough Act.

ctyazk3w8aa_xn0

Millardayo.com & Ayo TV ilimtafuta na kuyaongea haya>>>>Kwanza namshukuru mwenyezi Mungu sana kuchaguliwa kwenye tuzo hizo zipo pekee yangu kuna Tekno kutoka Nigeria, Ycee kutoka Nigeria, Simi kutoka South Africa Emtee kutoka South Africa kwahiyo wote ni wasanii wakubwa na tunawania tuzo hiyo’

Ninachowaomba watanzania wanipigie kura za kutosha sana binafsi namshukuru kwani miezi kama sita au saba kwenye muziki wa Bongo Fleva tangu nitambulishe wimbo wangu wa Kwetu na sasa mpaka nilipofika kwenye tuzo kubwa kubwa ni japo la kumshukuru Mungu sana’

Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Rayvanny akieleza furaha baada ya kutajwa kuwania MTV MAMA 2016

Soma na hizi

Tupia Comments