Habari za Mastaa

Taarifa juu ya kifo cha msanii Mbalamwezi, Muhimbili kuutambua mwili

on

Taarifa ya masikitiko iliyoripotiwa usiku wa kuamkia leo ni pamoja na hii ya kifo cha msanii wa kundi la The MAFIK aitwae Mbalamwezi ambapo toka usiku wa kuamkia leo baadhi ya marafiki na ndugu walifika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuthibitisha kuwa ni kweli mwili waliooneshwa ni wa Mbalamwezi ambae kabla ya hapo aliripotiwa kutojulikana alipo.

Baadhi ya ndugu wamesema taarifa za awali ni kwamba Mwili wake ulikutwa maeneo ya Africana Dar es salaam ukiwa hauna nguo ikiwa ni saa kadhaa zimepita toka msanii huyo atokomee bila kujulikana alipo.

Tupo hapa na tutaleta taarifa kamili zaidi muda mfupi ujao, pole kwa ndugu Jamaa na marafiki kwa msiba huu wa ndugu yetu Mbalamwezi. 🙏🏿 RIP Mbalamwezi.

Bonyeza PLAY hapa chini kusikiliza zaidi.

Soma na hizi

Tupia Comments