Stori Kubwa

Kingine kilichonifikia kuhusu wageni kufanyiwa vurugu na kuuawa South Africa..

on

Chaos SAImekaa kwenye HEADLINES ya story kubwa kutoka Afrika Kusini.. hii sio mara ya kwanza kutokea tukio la wageni yani watu ambao sio raia wa Afrika Kusini ambao wanaishi ndani ya nchi hiyo kufanyiwa vurugu, wengine kuuawa na watu ambao ni raia.. Hii imejirudia tena.

Mitandaoni kuna picha na video ambazo watu wametumiana zikionesha wageni hao wanavyofanyiwa vurugu ikiwemo kupigwa na kuuawa, wengine ni watoto wadogo kabisa.. ripoti ya mwisho kusikika jana imesema kuwa watu waliouawa katika vurugu hizo ni watu watano, japo hakuna ripoti ya raia yoyote wa Tanzania ambaye amejeruhiwa au kuuawa.

Mtanzania ambaye nimeongea nae toka Johannesburg Afrika Kusini amesema Johannesburg kuna hofu tu ya wageni kufanyiwa fujo lakini hakuna tukio la mtu yoyote kuvamiwa.. wahamiaji wanajifungia ndani, ukikutana na raia wenyewe wanakusalimia wakijua kuwa ni mgeni wanaanza kukufanyia vurugu, wengine wanapita kwenye maduka ya wageni na kuwavamia.

Vyombo vya habari vimesema Durban kuna machafuko makubwa zaidi ya vurugu hizo.

Kila kitachofikia nitahakikisha kinakufikia mtu wangu, hii stori ilikuwa #10 kwenye AMPLIFAYA APRIL 15 2015.

millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye FacebookTwitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments