AyoTV

“Sasa hivi tumeweka sheria mpaka majipu yanajitumbua yenyewe” – JPM

on

Leo July 10, 2017 Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alitembelea na kuzindua nyumba 10 za wahudumu wa afya katika kijiji cha Mkungo, Wilaya ya Chato, Geita zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation.

Akihutubia katika uzinduzi huo Rais Magufuli aliipongeza Taasisi ya Mkapa akisema anazipenda Taasisi zinazofanya kazi ya kuonekana na sio zinazoongea ongea.

“Mimi nazipenda sana Taasisi zinazofanya kazi kama hii ya Mkapa Foundation sio zinazotaka watoto wazae wakiwa shule. Taasisi za kila siku kwenye majukwaa mzinyime fedha, nataka Taasisi zinazofanya kazi inayoonekana sio za kuongea ongea tu.

“‘Hata mimi yupo mtoto wa mdogo wangu amezalia nyumbani, mtoto anamuita John, wa pili anamuita Samia lakini hakubakwa. Tunafanya ukaguzi nchi nzima kuwajua waliotumia vibaya fedha za pembejeo ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 1.5.” – Rais Magufuli.

Bonyeza Play kutazama Full Video

VIDEO: Benjamin Mkapa yuko Chato Geita, kapokelewa na JPM

Soma na hizi

Tupia Comments