Rais Magufuli leo July 25, 2017 ameendelea na ziara yake ambapo alikuwa katika Mkoa wa Singida alikozindua Barabara ya Manyoni – Itigi – Chaya yenye urefu wa km 89.3 ambapo mbali na kufanya uzinduzi huo alipata nafasi ya kuhutubia wananchi.
Nimekusogezea mambo 7 makubwa kati ya mengi aliyozungumza kwenye hotuba yake.
‘Pengine nikiondoka mimi hakuna atakayekuwa kama mimi, nasafisha njia ya Rais atakayekuja baada ya mimi’ – Rais @MagufuliJP
— millard ayo (@millardayo) July 25, 2017
‘Ni lazima niyatapike yote haya, nikikaa nayo nitapata presha bure, ila wale walioyafanya wakumbuke na madhambi yao’ – Rais @MagufuliJP
— millard ayo (@millardayo) July 25, 2017
‘Suala la ubinafsishaji mimi silipendi kabisa, siwezi nikawalaumu waliofanya hivyo lakini pia siwezi nikaacha kusema’ – Rais @MagufuliJP
— millard ayo (@millardayo) July 25, 2017
‘Nataka Tanzania hii iwe kama Ulaya na tutafika tu, lakini ili tufike huko ni lazima tutabanana kweli kweli’- Rais @MagufuliJP
— millard ayo (@millardayo) July 25, 2017
‘Wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya reli waanze kujiandaa kisaikolojia, wanaweza tu kuanza kubomoa taratibu nyumba zao’- Rais @MagufuliJP
— millard ayo (@millardayo) July 25, 2017
‘Niliporudishwa wizara ya ujenzi nilimfukuza Chief Executive Officer ndani ya siku 3 kwa sababu ya matumizi mabaya ya fedha’ – @MagufuliJP
— millard ayo (@millardayo) July 25, 2017
Wengine mmewachagua lakini wanaongelea ya mambo Dar es salaam tu kosea kuoa unaweza kutoa talaka lakini usikosee kuchagua – Rais @MagufuliJP
— millard ayo (@millardayo) July 25, 2017
“Matatizo yaliyopo kwenye uwezo wa Kiongozi na hakuyatatua, nalala mbele na huyo Kiongozi” – JPM