Michezo

Pigo kwa Brazil Neymar kuikosa Copa America

on

Timu ya taifa ya Brazil leo imetoa taarifa za kusikitisha kuhusiana na mshambuliaji wao anayeitumikia pia club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Neymar Jr.

Brazil wametoa taarifa kuwa watamkosa staa huyo kutokana na kupata majeraha ya kifundo cha mguu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Qatar ambao walikuwa wanautumia kwa maandalizi ya Copa America.

Neymar alikuwa anatarajiwa kuiongoza timu ya taifa ya Brazil katika michuano hiyo ila baada ya kufanyiwa uchunguzi amebainika kuwa ameumia kwa kiwango kikubwa katika kifundo chake cha mguu.

Soma na hizi

Tupia Comments