Ndani ya bunge la Afrika Kusini kwa mara nyingine imetokea hii ya Wabunge wa upinzani kumtaka Rais Jacob Zuma kutoka nje ya ukumbi wa bunge kwa madai kwamba amepoteza heshima na hana uhalali wa kulihutubia bunge la nchi hiyo kutokana na kashfa mbalimbali dhidi yake.
Kiongozi wa kambi ya upinzani Afrika Kusini Julius Malema alianza kumuagiza Zuma Kutoka nje na kuungwa mkono na Wabunge wengine ambapo Spika aliwatuma walinzi kumtoa nje kiongozi huyo kitu ambacho Wabunge wa upinzani hawakukipenda na kuamua kuanzisha vurugu ndani ya bunge.
Nimekuwekea hapa video fupi ya kilichotokea bungeni.
Wabunge wa upinzani Afrika Kusini walimtaka Rais Jacob Zuma atoke nje, Spika akazuia wakaanzisha vurugu na kupigana na askari ndani ya bunge pic.twitter.com/kYcsgIi4XY
— millardayo (@millardayo) February 10, 2017
Ili usipitwe na Breaking NEWS zote za Tanzania na nje ya Tanzania, matukio ya habari za mastaa, michezo na mengine, usiache kujiunga na Millard Ayo kwa ku-subscribe Youtube jina la “millardayo” pia Install APP ya “millardayo” kwenye Android na IOS, Facebook, Twitter na Instagram @millardayo
VIDEO: Tazama kilichofanya Wabunge wa upinzani Tanzania kutoka nje ya bunge juzi