Upelelezi wa kesi moja kati ya tano zinazomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya Hai Lengai ole Sabaya umekamilika na ameanza kusomewa maelezo ya awali katika Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha.
Upelelezi uliokamilika ni wa kesi ya jinai ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Katika shauri la Unyang’anyi wa kutumia silaha linalowakabili washtakiwa Lengai Ole Sabaya (34), Sylvester Nyegu(26)Mkazi wa Sombetini Arusha na Daniel Mbura(38) upelelezi wake umekamilika na Watuhumiwa wamesomewa maelezo ya awali na Kesi hiyo inatarajia kuanza kusikilizwa Julai 2 mwaka huu.
Wakili mkuu wa Serikali Tumaini Kweka akisaidiana na wakili Mwandamizi,Abdalah Chagula na Tarcilla Gervas aliiomba mahakama hiyo kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao kwa kuwa upelelezi umekamilika.